Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yazitaka nchi kufungua mipaka na kuruhusu kupita kwa wakimbizi kutoka Syria

UNHCR yazitaka nchi kufungua mipaka na kuruhusu kupita kwa wakimbizi kutoka Syria

Huku idadi ya raia wa Syria wanaotafuta hifadhi barani Ulaya ikizidi kuongezeka, Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na changamoto wanazopitia wakati ya safari zao. Alicekariuki na maelezo zaidi.

 (TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Hii ni pamoja na matukio ya kushamgaza ya mamia ya Wasyria wanaozama baharini. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limehusunishwa na habari kwamba ni watu 200 tu waliosurika ajali ya mashua iliyokua imewabeba kati ya watu 400 na 500 raia wa Syria na Palestina wakati ilipozama kwenye bahari ya Mediterranean tarehe 11 mwezi huu.

UNHCR inasema kuwa huenda ajali hiyo ilisababishwa na  uharibifu uliotokea kwenye mashua baadaa ya mashua yenyewe kushambuliwa kwa  risia ilipokuwa ikiondoka nchinilibyaambapo pia abiria wanne walijeruhiwa. Idadi kubwa ya raia wa Syria wamevuka bahari ya Mediterranean kutoka Misri na Italia. Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(CLIP YA MELISA FLEMING)

Serikali ya Misri inakadiria kuwa kati ya raia 250,000 na 300,000 kutoka Syria  kwa sasa wanaishi nchini Misri ambapo 122,774 wameandiskishwa na UNHCR.