Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko Agok yasababisha maelfu kumiminika Abyei: Ocha

Mafuriko Agok yasababisha maelfu kumiminika Abyei: Ocha

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema  maelfu ya watu wanazidi kumiminika mjini Abyei kutokana na mafuriko huko Agok, ambapo tangu mwezi uliopita hadi sasa idadiyaoimefikia zaidi ya Elfu Tatu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari mjiNew Yorkkuwa jamii kwenye eneohilozimeratibu usafirishaji wa raia kutoka Agok kwenda Abyei lakini hali mbaya ya barabara inasababishwa magari yashindwe kupita na hivyo kumaanisha kwamba kuna watu waliokwama Argok na katika vituo vingine. Hata hivyo amesema..

 (Sauti ya Martin)

 “Mashirika ya misaada yamesambaza vifaa vya kutumia nyumbani kwenye maeneo ya muda katika barabara ya Agok-Abyei na mji wa Abyei wenyewe kuhakikisha wanaowasili wana makazi, maji safi na salama, vyandarua na vifaa vingine muhimu. Wabia wa usaidizi wa binadamu wanapanga pia kusambaza chakula kwenye vituo vya muda kwa watu walio hatarini zaidi.

 Katika hatua  nyingine, Martin amesema Mkuu wa OCHA Valeria Amos yukoJamaicakwa ajili ya kuhudhuria mkutano kuhusu usaidizi wa kibinadamu.