Maadhimisho ya miaka 60 ya UM yaanza nchini Tanzania

17 Oktoba 2013

Wizara ya Mambo ya Nje kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa imeandaa mkutano wa vyombo vya habari ikiwa ni mwanzo wa wiki ya Umoja wa Mataifa, kumulika masuala muhimu kuhusu maendeleo, mafanikio na changamoto zinazoikabili nchi hiyo. Kauli mbiu ya wiki ya Umoja wa Mataifa mwaka huu ni “Mustakhabali tunaoutaka”.

Maadhishimo ya miaka 68 ya Umoja wa Mataifa yaliyoanza rasmi leo na kufikia kilele chake Oktoba 24 yanafanyika huku pande zote mbili serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa zikoihaidi kuendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

Umoja wa Mataifa kwa sasa umekuwa ikiteleleza mpango wake wa maendeleo kwa baadhi ya nchi za Kiafrika mpango unaofahamika kama UNDAP ambapo Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayonufaika na mpango huo.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa Tanzania imekuwa mshirika mkubwa wa Umoja wa Mataifa na ili kudhihirisha namna pande hizo mbili zinavyoendelea kutegemeana kumeandaliwa mikakati mbalimbali ya ushirikiano ambayo baadhi yake tayari imeanza kutekelezwa.

Kuhusu maadhimisho hayo ya wiki ya Umoja wa Mataifa, Kacou amesema kuwa kunatazamiwa kuandaliwa shughuli mbalimbali ikiwemo mdahalo wa wazi utakaofanyika katika chuo kikuu cha dare s salaam ambao utawahusisha watu wa kada mbalimbali.

Pia kunatazamiwa kufanyika maonyesho maalumu kuhusiana na kazi zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania