Hewa tuvutayo inchangia maradhi ya saratani:IARC

17 Oktoba 2013

Shirika la kimataifa kwa ajili ya utafiti wa saratani IARC limesema hewa inayovutwa na binadamu imechafuliwa na mchanganyiko wa chembechembe zinazosababisha saratani kama inavyoarifu taarifa ya Grace Kaneiya

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Wakala huo wa utafiti IARC unasema kuwa ijapokuwa inafahamika wazi kwamba kuvuta hewa hewa iliyochafuka inaweza kusabisha matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo matatizo ya kushindwa kupumua vyema na matatizo ya moyo, lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kuongezeka kwa matatizo mengine.

Utafiti huo unasema kuwa kuvuta hewa chafu kunaweza kusababisha mtu kupata matatizo ya saratani ya mabafu na saratani ya kibofu cha mkojo.

Wakala huo umesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2010, zaidi ya vifo 223,000 vilivyotokana na magonjwa ya saratani, vingi vyao vilisababishwa na uvutaji wa hewa chafu. Dr Dana Loomis ni wa wakala huo IARC.

(Sauti ya Dkt. Dana) TAfsiri itasomwa huku

Kumekuwa na ongezeko kubwa la viwanda katika nchi zinazoinukia kiuchumi huko Asia na Amerika ya Kusin. Watu wengi wanaufahamu wa kutosha juu ya kuongezeka kwa kiwango cha uchafuzi wa hewa nchini China. China imechukua hatua kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa lakini katika ukweli wa mambo wao siyo pekee yao wanapaswa kuhakikisha hewa haichafuliwi.Hili ni tatizo kubwa linalozikabili nchi ambazo zinachomoza kwa kasi katika sekta za viwanda duniani kote. Uchafuzi wa hali ya hewa ni tatizo kubwa linalosababisha athari nyingi kwa afya."

Katika hatua nyingine IRAC inasema kuwa kunauwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa matukio mapya ya watu kukumbwa na matatizo ya saratani hadi kufikia watu milioni 25 katika kipindi cha miaka 20 ijayo na wengi wao watatoka katika nchi zinazoendelea .