Wanawake wanajukumu kubwa kwa usalama wa chakula:Cousin

16 Oktoba 2013

Kuwawezesha wanawake ni suala muhimusanakatika kukabiliana na njaa na utapia mlo amesema Ertharin Cousin, mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Bi Cousin ameyasema hayo mjini Roma wakati wa hafla ya siku ya chakula duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 16, na mwaka huu kauli mbiu ni “mifumo endelevu ya chakula kwa ajili ua usalama wa chakula na lishe.”

Ameongeza kuwa hatua yoyote ya kuimarisha na kufanyia mabadiliko mifumo lazima zitambue pia jukumu kubwa na muhimu linalobebwa na wanawake kwani wanajukumu kubwa saana katika mifumo ya chakula.

Bi Cousin amesema mwaka jana WFP imewasaidia watu karibu milioni 100 walioathirika na migogoro,majanga na kushindwa kwa mifumo ya chakula katika mataifa na nchi zaidi ya 80.