Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya bora kwa mtu hutegemea mazingira bora ya chakula:WFP

Afya bora kwa mtu hutegemea mazingira bora ya chakula:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP limeelezea kile linachokiita mzunguko wa usambazaji chakula kwa kusema kuwa wakati mwingine unapotizama namna chakula kinavyolimwa, kinavyo uzwa sokoni, na kisha kusambazwa ni jambo la “kutisha”

 Shirika hilo ambalo linasisitiza kuwa, afya bora kwa mtu hutegemea mazingira mazuri ya chakula chenyewe, limesema kuwa maeneo mengi ambayo hulimwa chakula ni makavu na hayafai kwa kilimo hicho.

Limesema kuna wakati wakulima wenyewe hukosa mbinu bora za kuendesha shughuli zao na pia huandamwa na ukosefu wa masoko ya uhakika jambo ambalo mwishowe linaathiri mfumo mzima wa usambazaji chakula.

Likilielezea zaidi kuhusiana na hali ya kukabiliana na ukosefu wa chakula duniani, WFP imesema kuwa iwapo kuna watu zaidi ya milioni 842 wanaukosefu wa chakula, dawa siyo kwenda kuwasambazia chakula cha msaada bali ni kuhakikisha kwamba mifumo ya wakulima wadogo wadogo inazalisha vyema kwa kuzingatia viwango bora.