Tuendeleze azma ya Mwalimu ya kupata suluhu bila kumwaga damu: India

14 Oktoba 2013

Ni jambo la muhimu sana kutambua kuwa uhuru wa iliyokuwa Tanganyika kama ilivyokuwa kwa India ulipatikana bila kumwaga damu, na hiyo ni jambo la kujifunza jinsi Mwalimu Nyerere alivyoweza kushawishi kupitia mashauriano na mazungumzo hadi nchi yake kupata uhuru.

Ni kauli ya Mwakilishi wa Kudumu wa India kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Asoke Kumar Mukerji katika hafla maalum ya kumuenzi Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika mjini New York.

(Sauti ya balozi)

“Katika dunia ya leo, nafikiri jambo moja ambalo linajitokeza ni umuhimu ambao tunapatia mashauriano, mijadala, ushirikishi na mazungumzo katika harakati za kisiasa. Hakungalikuwepo na kumbukumbu nyingine nzuri zaidi ya kufanyia shughuli hii hapa Umoja wa Mataifa katika kuzungumzia nafasi ya mwalimu Nyerere kama jabali la Afrika kwenye medani za kimataifa na kukumbuka hii dhima katika dunia imejikita katika jukumu la mashauriano na kufikia malengo ya uhuru wa kifikra na kuchukua hatua.”

Balozi Mukerji akaenda mbali zaidi kugusia uhusiano wa India na Tanzania hususan suala la kujitegemea ambalo amesema Mwalimu Nyerere alilihusisha na kile ambacho Baba wa Taifa la India, Mahatma Ghandi alikuwa akitekeleza …

(Sauti ya balozi)

“Hiki ni kitu ambacho kamwe hatusahau, umuhimu wa kujitegemea! Kwa sababu hakuna kitu muhimu zaidi kwa nchi mpya huru na zile zinazoibukia kuwa na hisia ya kwamba wamefikia maelngo yao kupitia mpango wa kujitegemea