Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yatosha sasa ajali hizi za wahamiaji-IOM

Yatosha sasa ajali hizi za wahamiaji-IOM

 Kufuatia ajali ya pili mfululizo ya boti iliyohusisha wahamiaji nchini Italia na kusababaisha vifo vya watu wapatao 34, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limealaani hatua hiyo na kusisitiza wito wao wa kuzitaka nchi za Ulaya kuepusha majanga hayo.

 Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amesema wahamiaji walio wengi wanaamua kutumia njia za usafiri wa amaji kufuatia kutopewa hifadhi na nchi zilizoendelea mathalani za barani Ulaya na hapa anaanza kuelezea tamko la IOM.

(Sauti Jumbe)

Mwishoni mwa wiki boti iliyokuwa na wahamiaji takribani 250 ilizama kwenye mwambao waSicilykilometa  120 kutoka kisiwa cha Lampedusa kwenye eneo la bahari ya Maltese nchini Italia.