Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yalaani vikali kushambuliwa kwa kambi ya wakimbizi

UNRWA yalaani vikali kushambuliwa kwa kambi ya wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limelaani vikali machafuko yaliyozuka katika kambi ya Dera’a iliyoko Kusini mwa Syria ambako wakimbizi kadhaa wameripotiwa kufariki dunia na pia wafanyakazi wa shirika hilo wamejeruhiwa.

George Njogopa na ripoti kamili.

(Ripoti ya George)

Machafuko yaliyoibuka Oktoba 12, mwaka huu yanadaiwa kusababisha vifo vya wakimbizi saba wa Kipalestina huku wengine 15 wakijeruhiwa.Watumisha wa UNRA katika kitengo cha afya wanaripotiwa kujeruhiwa vibaya kutokana na machafuko hayo .

Mkurugenzi wa UNRWA anayehusika na eneo la Syria Michael Kingsley-Nyinah, amelaani vurugu hizo akisema kuwa kuendelea kupoteza maisha ya wakimbizi wa Kipalestina na kitendo kisichokubalika wala kuvumiliwa.

UNRWA imerejelea mwito wake akizitaka pande zinazopigana nchini Syria kujiepusha na matumizi ya nguvu za silaha katika maeneo ambayo yanakambi za wakimbizi wa Kipalestina na yale yanayokaliwa na raia wa kawaida.

Mapigano hayo ya hivi karibuni mbali ya kugharimu maisha ya raia hao pia yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za shirika la UNRWA hatua ambayo imeweka ugumu kwa shirika hilo kutoa huduma zake katika baadhi ya maeneo.