Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa watoto wa kike bado changamoto kubwa

Elimu kwa watoto wa kike bado changamoto kubwa

Leo dunia ikiadhimisha siku ya mtoto wa kike kwa kauli mbiu ubunifu katika elimu kwa wasichana , bado elimu ni changamoto kubwa ambapo barani Afrika  na kwingineko wasichana wengi inasemekana wamekosa fursa za elimu kwasababu mbalimbali ikiwamo umaskini na mila potofu.

 Noel Thomson wa radio washirika Afya Fm kutoka MwanzaTanzania ametembelea kata ya Isamilo iliyopo mkoani humo na kutuletea simulizi ya mtoto  Veronica Marko mwenye umri wa miaka 17 aliyekosa fursa ya kujiunga kidato cha kwanza licha ya kufaulu darasa la saba. Ungana naye.

(Sauti makala)