Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yajikita katika kuhamasisha unawaji mikono

Tanzania yajikita katika kuhamasisha unawaji mikono

Umoja wa Mataifa umeitaja Oktoba 15 kila mwaka kuwa ni siku ya unawaji mikono duniani. Siku hiyo ambayo itaadhimishwa mnamo Jumanne wiki ijayo, iliwekwa ili kukabiliana na matatizo ya kiafya hasa uwezekano wa kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko.

Siku hiyo huadhimishwa kwa shughuli mbalimbali za usafi, ikiwemo kuyashirikisha makundi ya vijana, wanafunzi pamoja na wanaharakati wa mazingira ambao wanachukua jukumu kubwa la kuhamasisha umma juu ya unawaji wa mikono.

Basi katika makala hii mwenzetu George Njogopa anaangazia hali ya unawaji mikono nchini Tanzania na mikakati inayoendelea kuchukuliwa karibu uungane naye