Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyerere kuenziwa jumatatu kwa tukio maalum New York

Nyerere kuenziwa jumatatu kwa tukio maalum New York

Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa hii Joseph Msami amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake wa  kudumu katika UM  Balozi Tuvako Manongi na ameanza kwa kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo?

 (Mahojianao na Balozi Manongi)

Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kiitwacho JULIUS NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza kutokana na ugonjwa wa saratani ya  damu.