IOM yaongeza msaada Ufilipino baada ya kupata dola milioni 1

11 Oktoba 2013

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM liameanzisha mikakati ya kutoa misaada maeneo ya Mindanao kusini mwa Ufilipino baada ya kupokea  dola milioni moja kutoka kwa serikali ya Japan. Fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia watu walioathiriwa na  mapigano yaliyotokea kwenye mji wa Zamboanga. Shughuli hiyo itatetekelezwa kupitia ushirikiano na idara ya masuala ya jamii nchini Ufilipino pamoja na makundi ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Ufadhili huu wa Japan unafuatia ufadhili wa dola milioni moja kutoka kwa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa wiki  iliyopita.

Mradi huo utawanufaisha karibu watu 20,000 kwenye vituo vya uokoaji kwenye mji wa Zamboanga na bidhaa zisizokuwa chakula na makao ya dharura.