Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Nyerere kuadhimishwa Umoja wa Mataifa Jumatatu

Siku ya Nyerere kuadhimishwa Umoja wa Mataifa Jumatatu

Kwa mara ya kwanza kumbukumbu ya Baba wa Taifa laTanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itafanyika kwa mara kwanza makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi waTanzaniakatika Umoja wa Mataifa ambapo Mwakilishi wake wa  kudumu Balozi Tuvako Manongi anatoa ufafanuzi.

 (Sauti ya Balozi Manongi)

Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu kiitwacho JULIUS NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando.