Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yaipongeza Tunisia kupitisha sheria kutokomeza utesaji:

Ofisi ya haki za binadamu yaipongeza Tunisia kupitisha sheria kutokomeza utesaji:

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeipongeza serikali ya Tunisia kwa hatua iliyochukua katika kuelekea kutokomeza masuala ya utesaji. Bunge la nchi hiyo limepitisha sheria ambayo itaanzisha shirika litakalokuwa linasimamia utokomezaji wa masuala ya utesaji.

 Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamuTunisia imekuwa ni nchi ya kwanza kwa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini kuchukua hatua hiyo. Hatu ya Tunisia inafuiatia taifa hilo kuridhia mikataba ya utokomezaji masuala ya utesaji.