Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afurahishwa na kuachiwa huru kwa waziri mkuu wa Libya

Ban afurahishwa na kuachiwa huru kwa waziri mkuu wa Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amefurahishwa na kuachiwa kwa waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan na kusisitiza uungwaji mkono kwa serikali ya Libya huku akirejelea kulaani utekwaji nyara kwa kiongozi huyo.

Katika taarifa yake Bwana Ban amevitaka vyama mbalimbali na watu wa Libya kukubaliana katika vipaumbele vya taifa na kujenga nchi imara pamoja na kuheshimu utawala wa kisheria na haki za binadamu.

Bwana Ban pia amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unaunga mkono watu wa Libya katika nia ya kuunda taifa la kidemokrasia na kusonga mbele katika mabadiliko ya kisiasa . Ametaka jumuiya ya kimetaifa kusaidia Libya katika mchakato huo.