Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yazindua kampeni ya kadi nyekundu kwa ajira za watoto

ILO yazindua kampeni ya kadi nyekundu kwa ajira za watoto

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

Shirika la Kimataifa la Ajira, ILO, limezindua kampeni ya kusaidia kupiga vita ajira za watoto. Kampeni hiyo iitwayo, Kadi Nyekundu kwa Ajira za Watoto, imezinduliwa wakati wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ajira za watoto, ambalo limehitimishwa leo Oktoba 10 mjini Brasilia, Brazil.

Kampeni hiyo inalenga kutoa chagizo kwa umma kuchukua hatua kutokomeza ajira za watoto, huku ikitarajia kutumia michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwaka 2014 nchini Brazil kama uwanja wa chagizo hilo la kimataifa.

Kadi nyekundu katika kandanda hutolewa kwa mchezaji ambaye amekiuka sheria za kandanda, na kila inapotolewa, ni lazima aondoke uwanjani. Michuano hiyo ya kandanda itafanyika mjini Brazil.

Kwa mujibu wa ILO, kuna zaidi ya watoto milioni 168 walio kwenye ajira za watoto kote duniani, na watoto hao hufanya kazi mashambani, katika kuchimba migodi na viwandani. Wengi wengine hunyanyaswa katika biashara ya ngono na madawa ya kulevya.

Kampeni hiyo imeungwa mkono na wasanii na wanaharakati, wakiwemo waigizaji filamu Tim Roth, Susan Sarandon na Wagner Moura.