UM wapigia chapuo elimu ya mtoto wa kike

10 Oktoba 2013

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu limeanzisha mkakati ambao unazitaka serikali, mashirika ya kirai, sekta binafsi pamoja na watunga sera duniani kutoa kila kinachowezekana kwa watoto wasichana ili kuhakikisha dunia ina maisha bora kupitia elimu.

George Njogopa na maelezo kamili

TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Katika taarifa yao ya pamoja wataalamu hao wamesema kuwa, kutengwa kwa wasichana kwenye mifumo ya elimu, kunaweza kusabisha gharama kubwa kwa mtoto wa kike mwenyewe , familia na hata jamii kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na wataalamu hao ikiwa ni siku ya pili ya maadhimisho ya siku ya mtoto duniani ambayo yamezinagatia kuondolewa vikwazo vyote vya kielimu kwa watoto.

Kundi hilo la wataalamu limesema kuwa pamoja na kuwepo kwa hali ya matumaini hasa kwa kupungua kiwango cha wanafunzi wanaocha shule ambapo kiwango chao kimepungua kutoka watoto milioni 102 mwaka 2000 hadi kufikia milioni 57 mwaka 2011lakini katika ukweli wa mambo bado kuna pengo kubwa la wanafunzi wanaojiandikisha elimu ya msingi.

Wamesema kuwa watoto wa kike katika nchi zinazoendelea bado hawapewi fursa sawa za kujiunga na elimu ya msingi