Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kushughulikia ubora wa maji wazinduliwa mjini Budapest

Mpango wa kushughulikia ubora wa maji wazinduliwa mjini Budapest

Katika jitihada za kuboresha usimazizi wa maji duniani Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa ushirikiano na taasisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira na mradi wa kimataifa kuhusu maji wamezindua mpango unahusu viwango vya maji duniani kwenye mkutano kuhusu maji mjini Budapest. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Afya ya viumbe vya majini inazidi kuhatarishwa na kuendelea kudorora kwa ubora na viwango vya maji kutokana na athari za wanadamu, kutokuwepo kwa maendeleo endelevu, matumizi ya ardhi, usimamizi wa maji na mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa sasa viwango vya maji vilivyoko ni vile vya maji ya kunywa, maji ya kustarehe, ya unyunyisahi kwenye kilimo, kwa mifugo na mengineyo. Hakuna viwango vya maji vilivyowekwa kwa viumbe vya majini na lengo la mradi huo ni kuweka mipangilio mwafaka ya kuziwezesha tawala za kitaifa na kimataifa kuboresha usimamizi wa maji na viumbe vyake. Kwenye awamu ya kwanza ya mradi huo kundi la wanasayansi wa kimataifa watatoa mipangilio ambapo kundi lingine la watunza sera likiwemo Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa na washika dau wataunga mkono kazi ya wanasayansi hao.