Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuendelea kusaidia Haiti kukabiliana na Kipindupindu

UM kuendelea kusaidia Haiti kukabiliana na Kipindupindu

Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kila inachoweza kusaidia wananchi wa Haiti kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu, ni kauli ya Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq aliyotoa kwa waandishi wa habari mjini New York. Alikuwa akijibu swali kuhusu kesi ya madai iliyofunguliwa kwenye mahakama moja mjiniNew Yorkdhidi ya umoja wa mataifa juu ya watu walioathiriwa na kipindupindu nchini Haiti. Farhan amesema si mwenendo wa Umoja wa Mataifa kuzungumzia hadharani madai yoyote dhidi yake ikiwemo hilo la Haiti. Hata hivyo kuhusiana na ugonjwa wa Kipindupindu Haiti amesema Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali na wananchi kwa kuwapatia msaada wa hali na mali kwa waathirika pamoja na kuweka miundombinu stahili  na huduma kwa wote.