Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaidhinisha chanjo mpya dhidi ya kirusi kinachosababisha uvimbe kwenye ubongo

WHO yaidhinisha chanjo mpya dhidi ya kirusi kinachosababisha uvimbe kwenye ubongo

Shirika la afya duniani WHO limeidhinisha chanjo mpya dhidi ya kirusi kinachosababisha kuvimba kwa ubongo, Japanese Encephalitis na hivyo kuokoa maisha ya watoto wengi kwenye nchi zinazoendelea kama vile Kusini mwa Asia, China na Urusi ambako ugonjwa huo hupatikana zaidi. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kwa sasa hakuna tiba ya ugonjwa huu lakini unaweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo au kwa kuuguzwa hopitalini kama moja ya njia ya kuzuia vifo. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan amesema kuwa kuidhinishwa kwa chanjo hiyo ni mafaniko kwenye jitihada za kuwakinga watoto kwenye nchi zinazoendelea dhidi ya ugonjwa wa ubongo. Dkt. Chan ameongeza kusema kuwa chanjo zaidi zinazoundwa nchini China zitaidhinishwa na WHO na ulimwengu mzima utafaidika.