Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa kujieleza ni changamoto kwa kesi zinazowakabili wabunge:IPU

Uhuru wa kujieleza ni changamoto kwa kesi zinazowakabili wabunge:IPU

Muungano wa wabunge duniani IPU unaendelea na mkutano wake mjini Geneva na leo umeendelea na kikao chake ukitathimini na kuangalia uwezekano wa kupitisha azimio dhidi ya kesi zinazowakabili wabunge mbalimbali duniani. Assumpta Massoi na maelezo kamili

(RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Kwa mujibu wa IPU kesi nyingi za wabunge chanzo ni uhuru wa kukusanyika na kujieleza ambayo ni moja ya haki zao za msingi, lakini mara kadhaa imekuwa ikiwaweka matatani na wengine kujikuta rumande au jela. Hivyo IPU inasema kupitishwa azimio kusaidia kutatua kesi hizo ni muhimukamaanavyosema Anne  Clywd ni mbunge wa Uingereza na mjumbe wa kamati ya haki za binadamu ya IPU

(SAUTI YA ANNE CLYWD)

 “Leo katika mkutano wetu natumai tutakuwa tunapitisha azimio ya kesi zinazohusisha wabunge wa Uturuki, DR Congo, Burundi, Pakistan, Sri Lanka, Maldives , Bahrain, Colombia, Belarus na wengineo”

IPU imeongeza kuwa kesi nyingine inayowatia mashaka ni ya G11, inayohusisha wabunge 11 wa Eritrea waliokamatwa na kuswekwa rumande hadi leo hatmayaohaijulikani na ni sulba kwa familia zao.

 (SAUTI YA ANNE CLYWD)

“Miaka 12 iliyopita wabunge 11 wa Eritrea walikamatwa bila mashitaka baada ya kuandika barua ya wazi wakitaka mabadiliko nchini humo , wanashikiliwa pasipofahamika na hatma yao haijulikani. Leo tutasema wazi kwamba serikali ya Eritrea imekiuka haki za binadamu ya wabunge hao 11”