Nzige, hali ya hewa vyasababisha uhaba wa chakula nchini Madagascar

9 Oktoba 2013

Nchini Madagascar hali ya chakula si shwari kwa tu Milioni Nne waishio vijijini ambapo Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umesema baa la nzige na hali mbaya ya hewa vimepunguza mavuno ya mchele na mahindi, vyakula vikuu nchini humo. Watu wengine Milioni Tisa nukta Sita wako hatarini kukabiliwa na uhaba huokamaanavyoripoti Alice Kariuki.

 (Taarifa ya Alice)

 Hali hiyo ya kuwepo kwa ukosefu wa chakula imeibuliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la mpango wa chakula duniani WFP na Shirika la chakula na kilimo FAO, yaliyoendesha tathmini katika kipindi cha mwezi Juni na Julai mwaka huu. Mashirika hayo yametaja sababu ya kujitokeza kwa hali hiyo ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa yaliyojitokeza mwaka uliopita. Madagascarilikumbwa na kimbunga kikubwa kilichovuruga maeneo mengi muhimu na kusababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu na kuharibu shughuli za kilimo.  Ama kujitokeza kwa wadudu waharibifu aina ya Nzige kulisababisha wakulima wengi kuvunjika moyo kuendelea na shughuli zao. David Orr ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA DAVID ORR)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter