WFP yakumbwa na ukata kusaidia wakimbizi wa ndani DR Congo

8 Oktoba 2013

Kwa mujibu wa tathmini ya awali, Shirika laKimataifa la Mpango wa chakula WFP, linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vitenda kazi ili kukabiliana na matatizo yanayoendelea kujitokeza Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, hatua ambayo imelifanya kuchukua chakula kutoka katika maeneo mengine na kupeleka huko. George Njogopa na maelezo kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)Kwa kuzingatia kiwango cha watu wanaendelea kukosa makazi, WFP inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 4.2 ili kukidhi mahitaji ya dharura katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa. Hata hivyo ili kuwakirimu waathirika hao, WFP inasema kuwa inalazimika kusaka chakula kwa watu wanaokadiriwa kufikia  80,000 kiwango ambacho kinaweza kubadilika na kufikia 120,000.

Kuna wasiwasi huenda hali ikawa mbaya zaidi katika siku za usoni kutokana na mapigano yanayoripotiwa kuendelea katika maeneo mbalimbali. Katika baadhi ya maeneo imekuwa vigumu vikiwa kutokana na mapigano hayo ambayo yanagharimu maisha ya raia wasiokuwa na hatia.  Mashirika kadhaa ya kiraia hata hivyo yamefanikiwa kupenya hadi kwenye maeneo korofi na kuwezesha huduma za utoaji wa misaada. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)

 “Ili kusaidia watu hao waliopoteza makazi, WFP  inahitaji kusaidia watu Elfu Themanini wanaohitaji msaada na hivyo  badi inahitaji msaada wa dola Milioni 4.2 kwa kuwa hatuna tena fedha za kushughulikia janga hilo na hivyo tumelazimika kutumia akiba kutoka operesheni nyingine.”