Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la raia wa Sudan Kusin waliokwama Renk sasa waanza kurejeshwa

Kundi la raia wa Sudan Kusin waliokwama Renk sasa waanza kurejeshwa

Meli kubwa ya mzigo ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, imeondoka huko Sudan Kusin ikiwa imechukua wahamiaji 947 waliokuwa wamekwama katika eneo la Renk tangu mwaka 2011.

Meli hiyo inatazamiwa kutua nanga katika mji wa Juba katika kipindi cha siku zinazokadiriwa 15 tangu iondoke huko Oktoba 4.

Itapowasili Juba, raia hao wanatazamiwa kupatiwa fedha na mahitaji mengine muhimu yatayowawezesha kuelekea katika maeneo yao .

Mpaka wa mji wa Renk ulioko Sudan Kusin katika jimbo la Upper Nile,kituo cha kukusanyika kwa mamia ya raia wanaorejea kutoka Sudan.

Kuondoka kwa idadi kubwa hiyo ya raia, kunafanya jumla ya wale wote walioondoka katika mji wa Renk kufikia 11,000, na kati ya hao 6,600 wanahitaji suluhisho la muda mrefu.