Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha msaada wa dharura kwa waathiriwa na mzozo nchini Ufilipino

UM waadhimisha msaada wa dharura kwa waathiriwa na mzozo nchini Ufilipino

Mfuko wa masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) imetoa dola milioni tatu  zitakazowasidia watu wa Samboanga walio kusini mwa Ufilipino walioathiriwa na mzozo hivi majuzi.

Mzozo huo umewalazimisha watu 125,000 kuhama nmakwao nusuyaowakiwa wamechukua hifadhi  kwenye vituo uokoaji. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibiadamu OCHA inasema kuwa nyumba za zaidi ya familia 10,000 zimeharibiwa kabisa na mafuriko siku chache zilizopita. Msemaji wa OCHA mjini Geneva Yens Laerke anasema kuwa mvua nyingi zinazonyesha zimeharibu makao ya muda na kuathiri zaidi hali ya wale waliohama makwao.

(SAUTI YA YENS LAERKE)

Msaada wa CERF unapitia mashirika ya Umoja wa Mataifa na IOM kuweza kuhudumia mahitaji ya usimamizi wa kambi, maji , usafi, usalama, usalama wa watoyo,dhuluma zinazohusaina na jinsia afya ikiwemo afya ya uzazi, chakula na bidhaa zisizo chakula kama vyombo vya kupika. Hali kwenye vituo vya uokoaji ni misongamano kwa kuwa watu walioathiriwa na mzozo waliokuwa wamerudi makwao na wale ambao wameathiriwa na mafuriko kwa sasa wamerejea kwenye vituo hivyo. Msaada wa CERF unasaidia kuchukua hatua za haraka za idara za serikali na utawala.

Mashirika ya kibinadamu nchini Ufilipino yanaomba dola milioni 24 kwa oparesheni zote za kibinadamu ambazo zinatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miezi sita.