Tubadili fikra tuweze kufanya biashara miongoni mwetu: Tanzania

8 Oktoba 2013

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo leo umeingia siku ya pili na mwisho ambapo wajumbe wanajadili jinsi ya kuhakikisha fedha zinapatikana kutekeleza shughuli za maendeleo. Joseph Msami na ripoti kamili.

 (Taarifa ya Joseph Msami)

 Katika mkutano  huo nchi zinazoendeleaTanzaniaimeeleza kuwa imeweka mikakati ya ndani ya kujipatia fedha za kufadhili sekta muhimu kwa maendeleo wakati huu ambapo ufadhili wa kigeni unasuasua. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mahadhi Juma Maalim amesemaTanzaniaina utaratibu uitwao Matokeo Makubwa Sasa ukiweka vipaumbele vitano ambavyo ni maji, nishati, miundombinu, elimu na ukusanyaji mapato. Amezungumzia pia majadiliano yaDohaya biashara yaliyokwama ambapo katika mahojiano maalum na idhaa hii, Naibu Waziri alielezea kile wanachofanya kujikwamua…

 (Sauti ya Mahadhi)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter