Miongo minne katika kifungo cha kutengwa ni mateso: Mtaalamu,UM

7 Oktoba 2013

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya vitendo vya utesaji Juan E. Méndez, ameitaka serikali ya Marekani kuondoa kifungo cha kutengwa alichowekewa Bwana Albert Woodfox  kilichowekwa tangu mwaka 1972. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) 

Bwana  Woodfox  pamoja na mwenzake Herman Wallace, walikumbwa na adhabu hiyo baada ya kutiwa hatiana kuhusika na mauwaji.Hata hivyo Wallace aliachiwa huru wiki iliyopita baada ya kushinda rufani yake.

Siku mbili baadaye yaani Oktoba 2 Wallace aliaga dunia baada ya kusambuliwa na saratani.Mpaka anaachiwa huru alikuwa ametumikia kifungo hicho cha upweke kwa miaka 41.

Akizungumzia adhabu hiyo, Bwana Mendez ameiita kama “ adhabu yenye kusikitisha na ambayo haina mwisho wowote”

Amesema kuwa adhabu ya namna hiyo ni utesaji mkubwa hivyo ameitaka Marekani kuchukua hatua za haraka kumwachia mfungwa huyo

Makundi ya kutetea haki za binadamu nayo yamekuwa yakiitolea mwito Marekani kuondokana na adhabu hiyo ambayo wameitaka kuwa ni ya kikatili.