Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wapya ikiwemo Somalia na Bhutan wakaribishwa IPU

Wajumbe wapya ikiwemo Somalia na Bhutan wakaribishwa IPU

Muungano wa mabunge duniani IPU umekaribisha wajumbe wapya ambao ni Bhutan na Somalia katika ufunguzi wa mkutano wake wa 129 mjini Geneva huku Misri ikisubiri kuwa na bunge tena kabla haijajiunga na tena na IPU.

Kujiunga kwa Somalia na muungano huo kuliidhinishwa baada ya kuchaguliwa kwa bunge Agost 2012 kama sehemu ya mchakato wa kipindi cha mpito kufuatia miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hii ni mara ya nne Somalia inajiunga na IPu tangu ilipofanya hivyo mara ya kwanza 1963. Bhutan kwa upande wake inajiunga na IPu kwa mara ya kwanza . Bunge lilianzishwa mwaka 2008 na kuchaguliwa tena kupitia uchaguzi Julai 2013 likiwa na jumla ya wabune 47. Na maendeleo ya hivi karibuni huko Misri yaliyoshuhudia kuvunjwa kwa bunge Julai 3 mwaka huu inamaanisha kwamba taifa hilo halina chombo kinachoweza kuwa mwanachama wa IPU, ili kuwa mwanachama wa IPU lazima nchi iwe na bunge linalofanya kazi.

IPU inasema itakuwa tayari kuikaribisha tena Misri kwenye chama baada ya uchaguzi wa bunge jipya kufanyika, lakini kwa sasa inapaswa kusubiri.

Ongezeko la Somalia na Bhutan inafanya jumla ya wanachama wa IPU kuwa 163.