UNECE yatoa ripoti kuhusu changamoto: usimamizi wa makazi na ardhi

7 Oktoba 2013

Takwimu zilizotolewa na Kamishna ya biashara ya Umoja wa Mataifa kwa Ulaya UNECE zinaonyesha kuwepo kwa tatizo kubwa la ukosefu wa nishati ya umeme kwa baadhi ya nyumba katika nchi za Ulaya na Asia ya Kati.

Ripoti ya kamishna hiyo inasema kuwa nyumba nyingi zinazokaliwa na vijana zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme kunakochangiwa na umaskini wa kipato.

Ripoti hiyo pia imezungumzia utayari wa mataifa kukabiliana na majanga ya dharura ambapo imesema kuwa kwa kiasi fulani Marekani imefanikiwa kukabiliana na hali hiyo ya kukabili majanga ya dharura.

Kwa mfano imesema kuwa katika mwaka 2012, majanga ya kimaumbile yalipoteza watu 180, na kuwaathiri wengine 90,000 hatua ambayo ililata madhara katika sekta ya kiuchumi .

Ripoti hiyo imefahamisha kuwa zaidi ya watu 237,000 walikosa makazi barani Ulaya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ikiwa ni sawa na watu 74,000 kwa mwaka 2012 pekee.

Ripoti hiyo ya utafiti yenye kichwa cha habari kisemacho “Changamoto na vipaumbele juu ya makazi na usimamizi wa ardhi katika ukanda wa UNECE” pia imesema kuwa nchi wanachama wa ukanda huu zimechukua hatua kuendeleza sera na kutekeleza miongozi iliyotolewa na UNECE ili kukabiliana na hali hiyo.