Ban atiwa mashaka na hali inayoendelea CAR

7 Oktoba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon atiwa hofu na hali inayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambayo ni ya machafuko, isiyotabirika na isiozingatia sheria. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI)

Ban amesema anatiwa woga na ongezeko la mashambulizi ya kulenga na ulipizaji kisasi dhidi ya Waislam na Wakristo ikiwemo matukio ya karibuni kabisa katika mihimili ya Bossangoa-Bossembele.  Amelaani vikali mashambulio hayo ambayo yanaweza kuchochea zaidi machafuko nchini humo. Katibu Mkuu amezitaka pande zote wakiwemo wapiganaji wa zamani wa Séléka na makundi mapya kujizuia na vitendo vya ghasia dhidi ya raia na pia kuheshimu haki za binadamu. 

Ameikumbusha serikali wajibu wake wa kuwafikisha kwenye mkono wa sheria waliohusika na mauaji na pia kuwalinda watu wote wa Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya ukiukwaji wa haki zao.