Hali ya walimu bado ni dhalili: UNESCO/ILO

4 Oktoba 2013

Tarehe Tano ya mwezi Oktoba kila mwaka ni siku ya walimu duniani. Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake, mathalani lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO na lile la kazi ILO unasema kuwa hali ya walimu bado ni dhalili, wanaishi maisha yasiyo na hadhi, na wakifanya kazi hiyo muhimu katika mazingira duni. Heshima ya walimu imetoweka licha ya kwamba jukumu wanalofanya ni haki ya msingi ya kila mwanadamu. Kila uchao ni migomo ya walimu wakidai haki zao. ILO inaonya kuwa bana matumizi ya serikali isilenge tu kupunguza matumizi kwenye sekta ya walimu kwani inaathiri utoaji elimu. Je hali iko vipi huko Tanzania na Kenya? Ungana na Joseph Msami katika makala hii ya wiki.

(PCKG ya JOSEPH MSAMI na JASON NYAKUNDI)