Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za kuwasaidia manusura wa ajali ya mashua zaendelea pwani mwa Italia

Jitihada za kuwasaidia manusura wa ajali ya mashua zaendelea pwani mwa Italia

Jitihada za kuwasaidia manusura kwenye ajali ya mashua pwani mwa kisiwa cha Lampedusa zinaendelea kwa sasa ajali ambayo iligharimu maisha ya raia wa Eritra kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Jason nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

UNHCR inasema kuwa idadi ya waliokufa kwenye ajali hiyo ya mashua pwani ya kisiwa cha Lampedusa imepanda hadi watu 111. Waathiriwa wote ni raia wa Eritrea isipokuwa raia mmoja wa Tunisia ambaye anaaminika kuwa mmoja wa kundi lililokuwa likiiongoza mashua . Kwa sasa kuna manusura 155 miongoni mwao watoto wa kiume 40 walio kati ya miaka 14 na 17 na wanawake sita. Kulingana na manusura hao mashua hiyo iliondoka nchini Libya siku 13 zilizopita ikiwa imebeba watu 500. Wanasema kuwa walipokuwa wakikaribia pwani ya Italia mitambo ya mashua ilisimama. Wakitumai kuwa wangeokolewa hata hivyo mashua za uvuvi zipita pasipo kuwapa msaada wowote. Kisha wakawasha nguo na blanketi moto ili wapate kuonekana na hapo ndipo mashua moja ya watalii ilipotuma ujumbe na baadaye watu hao wakaokole na walinzi wa pwani. Melissa Fleming ni msemajiwa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)