Robo tatu ya watu Mali wakabiliwa na upungufu wa chakula na na mahitaji mengine:WFP/IOM

4 Oktoba 2013

Huko Kaskazini mwa Mali, robo tatu ya wakazi wanakabiliwa na hatari ya ukosefu wa chakula. Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 1.3 watahitaji msaada wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014.

Tayari shirika la Umoja wa Mataifa la  mpango wa chakula WFP na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM yameanza kufanya tathmini kujua hali halisi ya misaada inayohitajika Alice Kairuki na taarifa kamili

WFP imesema kuwa inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 67 ili kutoa msaada wa chakula huku mashirika mengine ya utoaji wa misaada ya kibinadamu yakielezea mazingira magumu ya kuyafikia baadhi ya maeneo ukiwemo jimbo la Kidali.

Katika eneo la Gao, kiwango cha watoto wanaokabiliwa na matatizo ya utapiamlo kimeendelea kusalia cha juu. Kiasi cha watoto 22,000 wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo ikiwa ni wastani wa asilimia 3.5

Katika wakati huo huo Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kufanya tathmini ili kujua misaada inayohitajika kwa watu waliokosa makazi, wale waliorejea na jamii inahowahifadhi waathirika wa machafuko  katika vijiji 109 Kaskazini mwa Mali. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM afafanua zaidi.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)