Wakimbizi wa Syria na Wairaq wanaorejea wanaleta athari kubwa Iraq:IOM

4 Oktoba 2013

Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM iitwayo “Iraq- Athari za mgogoro wa Syria” inasema kwamba kuendelea kuingia kwa wimbi la wakimbizi wa Syria na kurejea nchini kwao kwa wakimbizi wa Iraq waliokuwa Syria kuna athiri nchi nzima lakini hasa jimbo la Iraq la Kurdishan kusababisha kuongezeka kwa changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira.

IOM inasema vita vya Syria vitakuwa na athari za kijamii na kiuchumi za muda mfupi na mrefu kwa jamii za Iraq zinazowahifadhi wakimbizi wa Syria ikiwemo upungufu wa kazi za wasio na ujuzi au wenye ujuzi kidogo na upungufu wa jamii na wakimbizi wanaorejea kupata pato la kutosha kwa ajili ya kukimu mahitaji ya familia zao.

Wengi wa wakimbizi wa Syria wapo Kaskazini na Magharibi mwa majimbo ya Iraq ya Sulaymaniyah, Dahuk, Erbil, huku idadi ndogo wakiwa Ninewa, Anbar naKirkuk.  Na wakimbizi wengine wachache wako katika maeneo mengine ya Iraq huku Wairaq wanaorejea nyumbani wamegawanyika nchi nzima wengi wakiishi na jndugu zao.

IOM inasema wakimbizi waSyria220,000,nchiniIraqni ndogoukilinganisha na mataifa jirani lakini kuwa Wairaq 50,000 ambao wamerejea kutoka Syria.