Pansieri ahitimisha ziara Yemen

3 Oktoba 2013

Naibu Kamishna wa tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu Flavia Pansieri amehitishima ziara yake ya nchini Yemen ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika eneo hilo  tangu ateuliwe kwenye wadhifa huo. Kabla ya kuwa kwenye wadhifa huo, Pensieri  aliishi nchini Yemen kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka 2004-2008 akiwa Mwakilishi mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa. George Njogopa na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Huku akiwa na hali ya furaha kurejea tena katika mji wa Sanaa alikoishi kwa miaka minne, Pansieri amesema shabaha kubwa ya ziara yake hiyo ilikuwa ni kukutana na viongozi wa serikali pamoja na washirika wengine kwa ajili ya kujadiliana hali ya haki za binadamu na hatimaye kupanga mikakati ya kuisaidia nchi hiyo iliyopo katika kipindi cha mpito. Pia alituami fursa ya ziara yake hiyo kuzindua ofisi ya ya kamishna ya haki za binadamu ambayo ilianza kufanya kazi tangu March 2012. Hadi sasa ofisi hiyo inawatumishi 12 wanaofanya kazi kote nchini. Akielezea zaidi hali ilivyo, Naibu hiyo alisema kuwa Yemen imepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ikikabiliana na wimbi la mabadiliko ya kisiasa. Mchakato wa kuwepo kwa duru la maridhiano kwa ajili ya kumaliza hali ya uhasama iliyozuka katika miaka ya hivi karibuni umefanikisha kulirejesha taifa hilo kwenye mkondo sahihi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter