Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge Tanzania wasema sasa yatosha, wachukua hatua kulinda ndovu na faru

Wabunge Tanzania wasema sasa yatosha, wachukua hatua kulinda ndovu na faru

Kutwa kucha idadi ya ndovu na faru inazidi kuporomoka barani Afrika. Takwimu zasema kuwa nchini Tanzania kila siku ndovu 30 huuawa kwa ajili ya menoyao. Kwa hali hiyo baadhi ya wabunge wameamua kusema sasa yatosha na wameunda kikundi maalum cha kunusu rasilimali za nchi ikiwemo wanyamaporindovu na faru. Je wanafanya nini kunusuru viumbe hao wanaoendelea kutowekaTanzania?Hilo ni miongoni mwa maswali ambayo Joseph Msami wa idhaa hiyo amemuuliza Athumani Mfutakamba mmoja wa wabunge 12 waliounda timu hiyo.