UNDP kufadhili miradi ya mabadiliko ya tabia nchini Afrika

3 Oktoba 2013

Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNDP limepokea msaada wa dola za Marekani milioni 43.63 kwa ajili ya kuzipiga jeki nchi zinazojitahidi kusonga mbele kimaendeleo lakini zinaandamwa na hali ya umaskini mkubwa.

Kiasi hicho cha fedha kitafadhilia maeneo yanayohusu mabadiliko ya tabia nchi na mifumo inayotumika kutoa angalizo la mapema barani Afrika.

Mpango huo umepangwa kutekelezwa katika nchi kumi ambazo ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Ethiopia, Liberia, Malawi, São Tomé and Príncipe. Nchi nyingine zipo kwenye mradi huo ni  Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.

 

Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa Utawala  Msaidizi wa UNDP Abdoulaye Mar Dieye, mpango huo unashabaha ya kuleta uelewa katika maeneo ya mabadiliko ya tabia nchi ili.