Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwapa uwezo akina mama na wasichana kunaweza kuleta maendeleo barani Afrika: UNFPA

Kuwapa uwezo akina mama na wasichana kunaweza kuleta maendeleo barani Afrika: UNFPA

Waakilishi kutoka nchi 52 kutoka bara la Afrika, mashirika ya Umoja wa Mataifa na karibu mashirika 200 ya umma pamoja na miungano ya vijana wamekusanyika kwenye mkutano kuhusu idadi ya watu na maendeleo kujadilia hatua ambazo zimepigwa, changamoto na mianya iliyopo katika kuafikia malengo wa shirrika la idadi ya watu na maendekeo la Umoja wa Mataifa.

Mataifa hayo yatatoa mapendekezo yanayoweza kuchochea maendeleo katika kuafikia malengo yaliyowekwa mjiniCairomwaka 1994 yanayoangazia masuala ya kijinsia na afya ya uzazi kwa wakina mama na wasichana. Mkutamo huo wa siku tano umeandaliwa kupitia ushirikiano wa muungano wa Afrika  na tume Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya  uchumi barani Afrika