Watu 82 waangamia kufuatia kuzama kwa mashua pwani mwa Italia

3 Oktoba 2013

Takriban watu 82 wameaga dunia baada ya mashua moja iliyokuwa ikiwasafirisha wahamiaji wenye asili ya kiafrika kuzama kusini mwa kisiwa cha Lampedusa nchini Italia kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mashua hiyo iliyotokea nchini Libya inaripotiwa kuwabeba zaidi ya wahamiaji 500 wengi kutoka nchini Eritrea. UNHCR inasema kuwa mashua hiyo ilishika moto ikiwa umbali wa nusu maili kutoka pwani ya kisiwa cha Lampedusa. Zaidi ya wahamiaji 140 wameokolewa lakini hata hivyo mamia ya wengine hawajulikani waliko. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Walinzi wa pwani wanataumbia kuwa kuna kati ya watu 400 na 500 kwenye mashua. Bado kuna watu wengi wasiojuliana waliko wakati huu. Kulingana na tunavyoelewa, abiria wanaonekana kutoka Eritrea. Eritrea ni moja nchi tatu ambazo tumoena watu wakitoka mwaka huu. Kulikuwa na watu waliokuwa wakitoka nchini Syria wakati mmoja na Eritrea upande mwingine. Hi inafikisha watu 32,000 waliowasili kwa njia ya bahari nchini Italia na Malta kati ya mwexi Januari na Septemba mwaka huu. Inaonyesha kuwa kwenye sehemu hii ya dunia eneo la Mediterranean limesalia njia kuu ya kuvuka bahari kwa wahamiaji na watu wanaotafuta hifadhi.

Tukio hilo ndilo la pili linahusisha mashua wiki hii kwenye pwani ya Italia baada ya watu 13 kuzama walipojaribu kupiga mbizi siku ya Jumatatu kutoka kwa mashua iliyokuwa ikiwasafirisha.