Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SADC,UM kuendelea kukuza usalama,utawala bora na kupambana na maafa.

SADC,UM kuendelea kukuza usalama,utawala bora na kupambana na maafa.

Umoja wa Mataifa na jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika , SADC, zimerejelea tena makubaliano ya masaidiano katika usalama, utawala bora na maafa. Joseph Msami na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Msami)

Hayo ni matokeo ya ziara ya Katibu Mtendaji mpya wa SADC Bi Stergomena Tax ambaye ameiambia idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum mjini New York kuwa amefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa umoja huo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukubaliana kuendelea kushirikiana kuimarisha ulinzi, kuzuia maafa na kuimarisha demokrasia hususani wakati wa uchaguzi, lakini kubwa lililojiri ni kuhusu amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

(Sauti Tax)

Katibu huyo Mkuu mtendaji wa SADC ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo akazungumzia kile anachotaka kukitimiza.

(Sauti Tax)