UNAMA kuhakikisha ushiriki wa wanawake uchaguziAfghanistan:

2 Oktoba 2013

Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi za kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao nchiniAfghanistan.

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi maalumu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo Ján Kubiš, mjini Kabul Jumatano. Alikuwa akizungumza na wanawake wanaharakati katika hafla ya kila mwaka inayohusiana na azimio la baraza la usalama linalozungumzia ushiriki wa wakanawake katika mchakato wa kisiasa baada ya suluhu ya migogoro.

 Mwakilishi huyo ameuelezea uchaguzi wa 2014 kama ni joha muhimu itakayotanabahi mustakhbali waAfghanistan. Huku akiheshimu kwamba mchakato lazima uongozwe naAfghanistanlakini amesema Umoja wa Mataifa hautoona haya kuweka bayana mtazamo wake endapo kutakuwa na mapungufu.

Kubiš  amesema Umoja wa Mataifa una mpango wa kutumia kila fursa itakayojitokeza kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika mchakato ambao unachangia amani, utulivu na maendeleo nchiniAfghanistan.