Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laridhia taarifa kuhusu hali ya kibinadamu Syria

Baraza la Usalama laridhia taarifa kuhusu hali ya kibinadamu Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha dharura hii leo limepitisha taarifa ya Rais wa baraza kuhusu hali Mashariki ya Kati hususan nchini Syria ikieleza masikitiko yake juu ya kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na kudorora kwa utoaji wa huduma za msingi za kibinadamu kwa wakimbizi walio ndani na nje ya Syria.

Kupitia taarifa hiyo, Baraza la Usalama linataka pande zote husika kusitisha chuki na kutoa fursa kwa operesheni za kibinadamu nchini humo na kueleza bayana kuwa suluhu ya mzozo huo ni kwa njia ya kisiasa. Halikadhalika imetaka kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria. Taarifa hiyo inazingatia pia hali mbaya ya wakimbizi ikiwemo kupata mahitaji muhimu na changamoto zitokanazo na uwepo wao nchi jirani kama vile Jordan, Lebanon na Iraq na hivyo imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kuchangia ombi la misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi hao.