Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji sio bidhaa wala chanzo cha matatizo ya kiuchumi na kisiasa: UM

Wahamiaji sio bidhaa wala chanzo cha matatizo ya kiuchumi na kisiasa: UM

Wahamiaji wanatazamwa kama bidhaa au chanzo cha matatizo ya kiuchumi na kisiasa badala ya binadamu, amesema Abdelhamid El Jamri, Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za wahamiaji wafanyakazi.

Kamati hiyo imetaka nchi zote kuungana katika mkataba wa kimataifa ambao unalinda haki za kundi hilo ikisema kwa kukubali mkataba huu haina maana nchi inawajibika kutoa matunzo maalum kwa wahamiaji wafanyakazi bali mkataba unaeleza viwango vya ulinzi wa binadamu wote ili wawe na umuhimu wakiwa uhamishoni.