Kupinga vurugu na ukatili kunahitaji ujasiri: Ban

2 Oktoba 2013

Leo Oktoba 2 ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Vurugu na Ukatili, na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi, shujaa wa uhuru wa India ambaye aliacha sifa ya kudai haki bila kutumia vurugu. Katika ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuchukua msimamo na kupinga wanaotumia vurugu na ukatili kuendeleza nia na imani zao kunahitaji ujasiri. Joshua Mmali ana taarifa zaidi

(TAARIFA YA JOSHUA)

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Ni midundo ya kihindi ambayo imesikika hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, katika hafla maalum iloandaliwa na ubalozi wa India kwenye Umoja wa Mataifa, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga vurugu, ambayo pia ni siku ya kuzaliwa kwa hayati Mahatma Gandhi.

Katika hafla hiyo, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, amesema ujasiri unahitajika katika kupinga vurugu na ukatili,kamavile unavyohitajika katika kuacha migogoro na kufanya mazungumzo ya amani. Bwana Ban amewataja mashujaa wengine, wakiwemo Martin Luther King Jr na Nelson Mandela,  ambao walisisitiza ujumbe wa kuendeleza utu wa mwanadamu na kupinga vurugu ili kuendeleza ulimwengu ambao watu wa tamaduni na imani tofauti wanaishi pamoja kwa misingi ya heshima na usawa.

“Kunatakiwa azma ili kupinga uovu, ubaguzi na ukatili, na kudai heshima kwa tofauti za watu na haki za kimsingi za binadamu. Kupinga vurugu na ukatili kunahitaji viongozi- katika mataifa, katika jamii na hata nyumbani- kukiungwa mkono na jeshi la watu jasiri ambao wapo tayari kudai amani, uhuru na haki.”

 Bwana Ban amesema Umoja wa Mataifa unashabikia utatuaji wa mizozo kwa njia ya amani, na kutokomeza aina zote za vurugu na ukatili, uwe wa vyombo vya dola au katika itikadi za kitamadunikamavile ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Kuutokomeza ukatili kama huo kunaweza kuanza na kila mmoja wetu- nyumbani, shuleni na kazini. Ukatili unaweza kuambukiza, lakini pia mazungumzo ya amani. Umoja wa Mataifa unaangazia kutokomeza umaskini. Umaskini ni uwanja unaokuza ukatili na uhalifu.”