HAI yawasaidia wakimbizi Kipalestina waliokuwa Syria na sasa wamehamia Jordan

2 Oktoba 2013

Mashirika mawili ya ustawi wa binadamu,lile la Human Appeal International lenye makao yake huko Emirate, Ajman na lile linalozingatia hali bora kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA yamekubaliana kuwapa msaada wakimbizi wa Kipalestina waliokokuwa wakiishi nchini Syria ambao sasa wamekimbilia nchi jirani ya Jordan.

Masharika hayo yamekubaliana kwa pamoja kuwaangazia wakimbizi hao kwa kuwasambazia huduma muhimu ikiwemo zile zinahusu usafi.

Idadi ya wakimbizi wa Kipalestina ambao wanatokea Syria kwenda Jordan sasa imefikia 9,105.Makubaliano hayo yanafuatia maombi ya UNRWA iliyotaka kuungwa mkono ili kuwakirimu wakimbizi hao.

Akikaribisha msaada huo, Mwakilishi wa UNRWA Peter Ford,alisema kuwa kutolewa kwa msaada huo ni jambo la kufurahia hasa wakati huu ambao raia wa Kipalestina ambao sasa wanageuka wakimbizi mara mbili wakiwa katika hitajio kubwa.