Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasema imezidiwa nguvu na ongezeko kubwa la wakimbizi

UNHCR yasema imezidiwa nguvu na ongezeko kubwa la wakimbizi

Kamishna wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR António Guterres amesema kuwa mamia ya watu wameendelea kukimbia makazi yao jambo ambalo linazidisha hali ya wasiwasi kwani idadi ya wakimbizi wanajitokeza sasa hajapata kushuhudiwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Kamishna huyo ameiambia Kamati ya Utendaji inayokutana kwa mkutano wake wa kila mwaka kuwa,ongezeko hilo la wakimbizi limezidi uwezo wa UNHCR.

Amesema katika kipindi cha mwaka huu pekee, kiasi cha wakimbizi waliokimbia Syria na zaidi ya milioni 1.5 huku mamia wengine wa wakimbizi wameendelea kuyakimbia makazi barani Afrika ikiwemo nchi za Mali, Congo DRC na Somalia.

Gutteres alikuwa akifungua mkutano wa Kamati Kuu ya UNHCR ambayo ndiyo inayoweka mipango pamoja na kupanga bajeti ya mwaka ujao wa 2014.