Meno ya ndovu, ugaidi ni vita ya kiamataifa :Kikwete

2 Oktoba 2013

Rais Jakaya Kikwete amesema ujangili wa pembe za ndovu na faru ni

tatizo la kimataifa linaolohitaji kutokomezwa kwa ushirikiano huku

akitaka mataifa makubwa kudhibiti soko la pembe hizo ,hatua ambayo

amesema inaweza kukomesha uwindaji haramu unaoathiri utalii barani

Afrika.

Katika mahojiano amaaluma na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya

radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, rais Kikwete ambaye pia

ameelezea hatari ya ugaidi nchini mwake na duniani kwa ujumla amesema

hata hivyo nchi yake imechukua tahadhari kujihami na mashambulizi

hayo.

Kwanza rais Kikwete anaanza kufafanua ukubwa wa tataizo la uwindaji wa

pembe za ndovu na faru.

(Sauti ya Kikwete)