Tuangalie maneno na vitendo vya Iran: Netanyahu

1 Oktoba 2013

Pazia la Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefungwa rasmi Jumanne mchana kwa hotuba kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ambayo kwa kiasi kikubwa ililenga masuala ya nyuklia ikigusiaIran. Bwana Netanyahu katika hotuba yake amesema anashindwa kujiaminisha kwa dhati kwa kauli za Rais wa Iran Hassan Rouhani alizotoa hivi karibuni kuhusu masuala kadhaa ikiwemo matumizi salama ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo na hata kusema kuwa iko tayari kufungua ukurasa mpya wa mahusiano na nchi nyingine.

(Sauti ya Netanyahu)

“Natamani tungaliweza amini maneno ya Rouhani, lakini lazima tuangalie vitendo vyake. Ni vitendo tofauti kabisa visivyo na aibu kati ya maneno ya Rouhani na vitendo, yashangaza sana!”

Bwana Netanyahu akasema diplomasia inaweza kupatiwa fursa nchiniIranili kile isemacho iendane na vitendo vyake lakini kile ambacho jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya ni..

(Sauti ya Netanyahu)

“Mosi, vikwazo viendelee, pili usikubali makubaliano nusu nusu, Tatu ondoa vikwazo pale tu ambapo Iran itaharibu kabisa mpango wake wa nyuklia. Marafiki zangu, Jumuiya ya kimataifa iko mtegoni,. Iwapo unataka kutokomeza mpango wa nyuklia wa Iran kwa usalama, basi endelea na shinikizo.”