Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utesaji magerezani wazidi kuongezeka Libya

Utesaji magerezani wazidi kuongezeka Libya

Ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu inasema  kuwa vituo vingi vya magereza  nchini Libyabado vinaendelea na mwenendo wa kutesa watu na kuwapa huduma zisizostahili. Alice Kariuki na taarifa kamili

(TAARIFA YA ALICE )

Ripoti hiyo imesema kuwa vitendo hivyo vya utesaji mara nyingi hufanyika wakati watuhuiwa wanapotiwa nguvuni na wakati mwingine katika kipindi cha siku za mwanzo za mahojiano ikiwa ni njia mojawapo ya kumtaka mtuhumiwa kukiri kosa ama kutoa taarifa zaidi.

Ripoti hiyo inasema kuwa watuhumiwa hushikiliwa huku wakinyimwa fursa ya kukutana na wanasheria wala familia zao. Ofisi hiyo ya haki za binadamu inasema kuwa kuna zaidi ya watu 8,000 wanaendelea katika maeneo yenye mizozo bila kuchukuliwa hatua zozote. Wengi wao wanaoshikiliwa wapo kwenye maeneo ambayo yanamilikiwa na vikosi vya kijeshi. Ravina Shamdasani ni afisa wa ofisi ya haki za binadamu.

(Sauti ya Ravina)

 

“Kuna wakati ambapo baadhi ya  askari wa vikosi vyenye silaha wamekubali na hata kujaribu kuhalalisha vitendo vya unanyasi dhidi ya wafungwa. UM unapendekeza kuwa vikosi vyenye silaha viharakishe mchakato wa kukabidhi wafunguwa kwenye mamlaka ya serikali, na wakati huo huo wachukue hatua za kulinda wafungwa dhidi ya mateso na vitendo vingine vya ukatili. UM pia unatoa mapendekezo kwamba mamlaka ya Libya ipitishe mkakati wa kuchunguza na panapofaa, kuwaachilia au kuwashtaki  wafungwa wanaohusika na migorogo, kwa lengo la kutekeleza sheria ya mpito iliowekwa. Wanapaswa pia kuongeza uwezo wa mfumo wa sheria unahusika na  makosa ya jinia ili kulinda wafungwa dhidi ya aina yoyote ya unyanyasi na kumalizana na hali ya kutokujali ukiukwaji unaoendelea.”